Jinsi ya kuirithi Zawadi ya Bure ya uzima wa milele
Je ubatizo inahitajika kwa ajili ya wokovu?
Mpendwa YAHUSHUA, Ninakupokea sasa uwe Bwana na Mwokozi wangu, Wewe ni Mungu ninayempenda. Ninaamini ulilipa deni la dhambi zangu katika Kalvari, ulikufa na kufufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu. Ninakuomba uje moyoni wangu, unisamehe dhambi zangu, unisafishe niwe safi kutokana na maovu yote. Ninajuta nimetenda dhambi, na ninageuka mbali na dhambi hizo. Asante kwa kunijaza na Roho Mtakatifu wako, na kwa kunipa hamu ya kukutumikia siku zangu zote za maisha yangu, na kuishi maisha yako kwangu, YAHUSHUA, ili utukuzwe! Asante kwa kunipa hamu ya kusoma Bibilia yako, na kunipa hekima ya kuifahamu. Asante kwa kunipenda na kuokoa roho yangu, na kuifanya Imani yangu kukua, ili siku moja nitakuwa nawe Mbinguni. Unijaze sasa na Roho Mtakatifu wako na kuniweka huru kutoka kwa yule mwovu. Kwa jina lako YAHUSHUA ninaomba! Unizaidie YAHUSHUA nikumbuke kwamba Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa YAHUVEH, na ulikuja kutuokoa SISI wenye dhambi, hiyo ndiyo sababu unaitwa MWOKOZI wetu. Amina
Soma hili ombi na usome tena mara nyingine, mara hii SIO na hekima ya kiakili bali hekima ya kimoyo, amini kwa IMANI, na ukumbuke YAHUSHUA sio tu MUNGU bali Yeye ni rafiki yako ya kweli! Anakujali sana, anakupenda sana, jinsi vile ulivyo. Anachukia dhambi, bali anakupenda WEWE, mwenye dhambi!
YAHUSHUA alilipa deni la dhambi zako, sasa haupaswi kujihisi mwenye huzuni au kujihukumu tena! Ungama dhambi zako kwa YAHUSHUA. Zitaje zote, halafu Umwambie kwamba umejuta, Umwombe akusamehe! Dhambi zako zote za hapo awali na sasa. Dhambi ni chochote ambacho umetenda au unatenda kisichompendeza YAHUVEH ambaye ni Takatifu. Hakuna mtu aliyemkamilifu! Ukumbuke hiyo!
Soma Agano Jibya na upate kujua YAHUSHUA ni nani . 1Yohana 3:16. Bibilia inasema ni lazima umkiri Yeye kama Bwana na Mwokozi ili naye akukiri mbele ya BABA. Usimwonee haya YAHUSHUA, naye hatakuonea haya. Uwambie wengine kwamba umemkubali YAHUSHUA wa Kalvari na Nazareti, leo! Malaika wote mbinguni wanashangilia kwa kuwa jina lingine limeongezwa kwa Kitabu Cha Uzima cha Mwana Kondoo!
Tushangilie pamoja nawe. Kama unahitaji Mchungaji, tuka na zaidi ya moja. Karibu kwa ukoo wa YAHUSHUA! TUNATARAJIA KUKUTANA NAWE MBINGUNI, KAMA SIO HAPA DUNIANI!
Mtumie Elisabeth Barua pepe na umjulishe kuhusu zawadi ya uzima wa milele uliourithi kutoka kwa YAHUSHUA Masihi wetu wa dhamana!
revholyfire@hotmail.com
Rudi kwa ukurasa wa Wokovu
Je ubatizo inahitajika kwa ajili ya wokovu?
Ubatizo, Mto wa Yordani
Mbatizwe. (angalia Matendo ya Mitume 2:38,39)
Kubatizwa ina maana ya kutumbukizwa katika maji. Kwa kawaida, mtu usimama katika maji, akatumbukizwa kwa maji ( na Mkristo mwingine), halafu akatolewa kutoka majini. Ishara ya hili tendo linaonekana katika Warumi 6:1-7 na mfano wake katika Matendo ya Mitume 8: 26-39
Watu wengine hawafikirii ya kuwa ubatizo ni sehemu ya kumpokea YAHUSHUA. Walakini, kitu kimoja ni wazi katika Bibilia. Kuamini na kubatizwa kila mara yako pamoja, haitawanyiki. Kwa hivyo, ni wazi ya kuwa ubatizo ni sehemu ya kumpokea YAHUSHUA. Tunakuhimiza utafute “kwa nini” ya ubatizo katika Bibilia. Mkristo wowote anaweza kukubatiza.
Kubatizwa kwa maji ni njia moja. YAHUSHUA alisema, “Yahana alibatiza kwa maji lakini YAHUSHUA anabatiza na MOTO wa ROHO MTAKATIFU!” Baada ya kupokea upatizo wa maji, basi TAFUTA ujazo wa MOTO wa ROHO MTAKATIFU! Hapa ndipo gharama za ROHO MTAKATIFU uingia! Hata hivyo, usiamini ya kuwa USIPOkuwa na hizo gharama na kuongea kwa ndimi mbalimbali, basi hautaenda Mbinguni! Funzo lingine la uongo! Kama ingekuwa hivyo, basi YAHUSHUA angesema wazi wazi ya kuwa yeyote asiyeongea kwa ndimi mbalimbali hataokolewa! Tena kama hii ingekuwa kweli, haingehitajika YAHUSHUA kupeana uhai wake na damu katika Kalvari! Ni Damu tu ya YAHUSHUA inayosafisha dhambi kwa wale wanaopokea hiyo ZAWADI kwa IMANI!
Makanisa mengine hufundisha ya kuwa KAMA mtu asipobatizwa, hata mtoto mdogo, basi mtu huyo HAWEZI kuenda Mbinguni! Kama hii ingekuwa kweli, basi kwa nini ilihitajika kwa YAHUSHUA kukufa katika Kalvari? Ubatizo ni ishara ya nje ya kuwa tunamfuata YAHUSHUA! Watoto wadogo hawawezi kuelewa hii vilivyo, kwa hivyo hawapazwi kubatizwa hadi watakapoelewa anayopazwa mtu kulipa ili kumfuata YAHUSHUA. Watoto wachanga wanapazwa kukabidhiwa, wala SI kubatizwa, kwa kuwa wanapazwa kukomaa kiasi ili wafanye uamuzi wao wenyewe.
Kwa hivyo, badala ya kuangalia ubatizo kama jambo ANALOPAZWA mtu kutenda, juu ya kumkubali YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi wao, ili kuokolewa…mtu anapazwa kuhitaji kulitenda hili, ili aajilie ujazo wa Roho Mtakatifu na kuwaonyesha wote ya kuwa wanajitambulisha na kifo na ufufuo wa Mwokozi wao, YAHUSHUA ha MASHIACH!